Kikosi cha Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC kitamkosa mshambuliaji wake mahiri Donald Ngoma ambaye anasumbuliwa na majeraha kwenye mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zanaco FC siku ya Jumamosi.
Msafara wa kikosi hicho utaondoka kesho (Alhamisi) jioni kuelekea nchini Zambia kwa Ndege ya Shirika la Kenya Airways.
Msafara wa Yanga SC utakuwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi.
Yanga inaelekea Zambia katika mechi ya marudiano baada ya mechi ya awali Jumamosi iliyopita kutoka sare ya 1-1 na Zanaco FC Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Post a Comment