MANCHESTER, England
WACHEZAJI wa
Manchester United wanachunguzwa kutokana na kuwepo madai ya kuhusika
katika kurekodi video ya mwanamke akimchezea mchezaji kingono kisha
video hiyo kusambazwa kwa wachezaji wengine wa timu hiyo.
Inaelezwa kuwa mabosi wa klabu hiyo ndiyo ambao wanafanya uchunguzi
huo baada ya kuenea kwa taarifa za chinichini kuwa video hiyo
inamuonyesha mwanamke huyo akifanya matukio ya kingono na mchezaji mmoja
wakati wakiwa maliwatoni kisha wakawa wanarekodiwa na mchezaji
mwingine.
Jina la mchezaji aliyekuwa akirekodi na yule aliyekuwa na mwanamke
huyo hayajatajwa huku ikielezwa kuwa mwanamke huyo ana umri wa miaka 20
na ushee.“Tukio hilo lilitokea kwenye ukumbi mmoja uliopo Manchester,
wakati wao wakichezeana chooni, kuna mchezaji mwingine alikuwa
akiwarekodi juu ya mlango,” kilisema chanzo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment