0










Kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, asubuhi hii kimekwea pipa kwenye Uwanja wa Ndege Kimataiafa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) kuelekea mjini Mbabane, Swaziland kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows.

Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Somhlolo, mjini Mbabane, Swaziland Jumapili hii.

Katika mchezo huo, Azam FC inahitaji sare yoyote au ushindi wowote ili kuweza kusonga mbele kwa raundi ya mwisho ya mtoano (play off) baada ya ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa awali na iwapo itafuzu itakutana na moja kati ya timu 16 zitakazokuwa zimetoka kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Post a Comment

 
Top