MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma za kuomba rushwa ya Shilingi Milioni 25 baada ya kuonekana hawana hatia.
Maofisa hao ambao ni Msaidizi wa Rais wa TFF, Juma Matandika na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa shirikisho hilo, Martin Chacha walifikishwa mahakamani baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwatia hatiani kufuatia madai ya kurekodiwa wakiomba rushwa ya Sh. milioni 25 kutoka kwa viongozi wa Chama Cha Soka Geita (GFA) ili kuisaidia timu yao kupata nafasi ya kupanda Ligi Kuu Tanzania.
Post a Comment