Kikosi cha Real Madrid chini ya kocha wao, Zinedine Zidane usiku huu kimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji Napoli.
Madrid wametinga hatua hiyo kwa kumla ya mabao 6-2 baada ya mechi ya awali kushinda kwa mabao 3-1 pia.
Mabao ya vigogo hao kwa Hispania yamewekwa kimiani na Sergio Ramos dakika ya 52, Dries Mertens aliyejifunga dakika ya 57 na Alvaro Morata dakika ya 90+1.
Bao pekee la Napoli limefungwa na Dries Mertens dakika ya 24.
Kwa ushindi huo, Real Madrid wameungana na Bayern Munich ambao nao wametinga robo fainali kwa kuitupa nje Arsenal kwa jumla ya mabao 10-2.
Post a Comment