0


Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho.
Na Mohammed Mdose
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho, amesema yupo tayari kuichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, iwapo Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) litamtaka afanye hivyo.
Sheria za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) zinaruhusu raia wa nchi fulani kuichezea timu ya taifa ya nchi nyingine, akipata uraia wa nchi hiyo na iwapo akiwa hajawahi kuichezea timu ya nchi yake halisi mchezo hata mmoja katika timu ya wakubwa.
Akizungumza na Championi Jumatano, kiungo huyo alisema kuwa kama ikitokea nafasi hiyo, hatasita kukubali kwani tangu zamani alikuwa na ndoto siku moja ya kucheza timu ya taifa ila kwa hali iliyopo Brazil hataweza kuifanikisha ndoto hiyo.
Alisema kuwa anajua wazi haitakuwa jambo rahisi kwake kuichezea timu ya taifa ya Brazil kwani nchi yao ina wachezaji wengi, tena wenye vipaji vya hali ya juu, hivyo hawezi kupata nafasi huko.
“Nitakubali kama wakiniambia kwani nina hamu ya kuchezea timu ya taifa, si unajua Brazil kuna makundi ya wachezaji wapo kwenye timu kubwa za Ulaya? Tena wanajua sana, hivyo siyo rahisi mimi kuichezea Brazil, lakini nikipata nafasi Tanzania nitafurahi sana,” alisema Coutinho

Post a Comment

 
Top