0









Takribani mashabiki 200 wa Klabu ya Arsenal Jumanne usiku waliandamana wakiwa na mabango ya kumtaka kocha wao Arsene Wenger aondoke klabuni hapo maana anaiharibu timu yao.

Mashabiki hao ambao walikuwa wakiitaka klabu kutomuongezea mkataba Mfaransa huyo pindi atakapomaliza huu wa sasa, wameandamana kabla ya mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich ambao nao wamepigwa tena mabao 5-1 na kutupwa nje ya michuano hiyo.

Wenger alijiunga na Arseanal tangu mwaka 1996 lakini siku za hivi karibuni ameonekana kuelemewa na kuishiwa mbinu za kupambana na timu pinzani na kuipa mafanikio timu hiyo yakiwemo makombe.

Post a Comment

 
Top