Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, inaungana na wapenzi wa soka nchini kuomboleza kifo cha kiungo nyota wa zamani wa Kimataifa wa Tanzania, Tanzania Prisons na Yanga, Godfrey Boniface 'Ndanje', aliyefariki dunia katika Hospitali ya Makandana, Tukuyu mkoani Mbeya.
Azam FC inawatakia moyo wa subira wanafamilia, ndugu, jamaa, mafariki na timu zote alizochezea kiungo huyo, katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raji'un.
Source: Azam FC
Source: Azam FC
Post a Comment