0

Zikiwa zimebaki siku nane (8) tu miamba miwili ya soka hapa nchini Simba na Yanga kukwaana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kikosi cha Wekundu wa Msimbazi 'Simba SC' leo kimeelekea visiwani Zanzibar tayari kuanza maandalizi ya mchezo huo utakaopigwa Februari 25, 2017.

Wakati Simba wakielekea Zanzibar, watani wao Yanga kesho watakuwa uwanjani kuwakabili Ngaya katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top