0


Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez yupo nchini Hispania kusikiliza kesi yake inayomkabili ya ukwepaji kodi wakati akiichezea klabu ya Barcelona.

Kocha wa Aresenal, Arsene Wenger ameeleza kuwa mbali na safari hiyo, staa huyo atarejea mapema na kesho Jumamosi atashiriki mazoezi na timu yake tayari kuwakabili Sutton United katika Kombe la FA.

Staa huyo raia wa Chile, mapema mwezi huu alikiri ukwepaji kodi wa £865,000 wakati akiichezea Barcelona.

Post a Comment

 
Top