0
Mshambuliaji wa Simba SC, Danny Sserunkuma akiwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar wakati wa mechi ya fainali Kombe la Mapinduzi usiku huu huko Zanzibar.
Patashika wakati wa mtanange huo.
Ramadhan Singano 'Messi' akijaribu kumtoka beki wa Mtibwa, David Luhende.
Mashabiki wakifuatilia mechi hiyo.
Kikosi cha Simba SC kilichoanza mechi hiyo.
Kikosi cha Mtibwa Sugar kilichoanza mechi hiyo ya fainali.
KLABU ya Simba imetwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa penalti 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya matokeo ya 0-0 katika dakika 90, usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Penalti za mabingwa hao mara tatu wa Kombe la Mapinduzi ziliwekwa kimiani na Awadh Juma, Hassan Kessy 'Danny Alves', Hassan Isihaka na Dan Sserunkuma huku za Mtibwa Sugar zikifungwa na Ally Lundenga, Shabaan Nditi na Ramadhan Kichuya.
Katika michuano hiyo, Simon Msuva wa Yanga ameibuka mfungaji bora akiwa na mabao 4, Salim Mbonde wa Mtibwa akichukua tuzo ya mchezaji bora huku kipa wa Mtibwa, Said Mohammed akiwa ndiye kipa bora wa michuano hiyo iliyomalizika usiku wa kuamkia leo.

Post a Comment

 
Top