0
Kocha wa Guinea ya Ikweta Esteban Becker amefurahishwa kupita kiasi na hatua ya wenyeji hao kufuzu kwa hatua ya robo fainali.
ikumbukwe kocha Becker alikabidhiwa kuiongoza klabu hiyo ikiwa zimebaki siku 11 pekee kabla ya kuanza michuano hiyo ambayo walikabidhiwa waiandae hapo mwezi novemba mwaka ulopita.

Wenyeji wamefuzu kwa hatua hiyo baada ya kuishinda Gabon 2-0 na kocha huyo amebainisha kwa kusema inafurahisha ni kama simulizi ya ‘Cinderella’ timu dhaifu inapofunga timu kubwa, nawapongeza kwa moyo wao wa kujitolea, upambanaji na hamasa na jitihada kuisaka heshima”

Awali, taifa hilo liliondolewa katika michuano hiyo kwa tuhuma za kumtumia mchezaji asiyestahili lakini hata hivyo walirejeshwa na kukabidhiwa uwenyeji wa michuano hiyo kufuatia kujitoa kwa taifa Morocco kwa kilichodaiwa hofu ya ugonjwa wa Ebola.
Ni nani Esteban Becker?
awali Esteban Becker alikuwa akifundisha timu ya taifa ya wanawake ya taifa hilo
katika viwango vya Fifa guinea ya Ikweta wanashika nafasi ya 118 lakini hiyo haikuwa kikwazo wao kumaliza nafasi ya pili katika kundi A lililoongozwa na Kongo.

“kikosi hiki kimeweekwa pamoja takribani siku 20 tu zilizopita huko Madrid, kisha tukaenda Lisbon na kukubaliana kupambana tukiwa na imani ya kusonga mbele” “tulipokuwa katika mafunzo tulijiaminisha kuwa tungefika mbali. Hata kufika hatua ya hii kwa taifa dogo kama letu ni heshima kubwa”
kikosi hicho chenye nyota 23, 14 kati yao wazaliwa wa hispania wakati watano ndio kwanza walianza kuitumikia nchi hiyo huko Lisbon katika pambano la kirafiki dhidi ya ya Cape Verde. akizungumzia pambano la juzi dhidi ya Gabon ambapo nyota wa zamani wa miamba ya hispania, Real Madrid Javier Balboa alifanyiwa madhambi katika eneo la kumi na nane na hivyo Guinea kupta penati ambayo nyota huyo aliifunga kwa ustadi mkubwa kocha huyo amepinga madai ya wapinzani wao ya kujirusha ili wapate penati na badala yake akasema “nina furaha na taifa langu, timu yangu na nafsi yangu” leo ni siku kubwa kwa wana Guinea ya Ikweta wote”.
kwa upande wake Balboa alisema “penati ile ilikuwa halali. Sikujirusha. Ni kweli ilibadili mchezo lakini ieleweke tulifunga mabao mawili”
awali kocha wa Gabon, Jorge Costa alisema “sitaki kujitetea ila ni wazi Ikweta wasingefunga kama siyo kupewa penati isiyostahili””si ndio tungekuwa wa kwanza kufuzu kwa hatua ya robi fainali, lakini Balboa amejirusha, nimekuwa katika soka kwa mda mrefu hivyo nalielewa hilo mimi sifanyi kazi supermarket.”
katika robo fainali Guinea ya Ikweta watapambana na vinara wa kundi B ambalo lilikuwa likijumuisha mataifa ya Tunisia, Cape Verde, DR Congo na Zambia, siku ya jumamosi

Post a Comment

 
Top