0
Na Baraka Mbolembole,
Azam FC walikuwa wa kwanza kufika katika eneo la Simba SC, lakini mpira uliopigwa hovyo na mshambulizi, Kipre Tchetche haukuwa na madhara. Baada ya dakika nne Simba ‘ wakauchukua’ mchezo, mlinzi wa kulia, Hassan Kessy alipanda na kupiga ‘ kiki kali’ kunako dakika ya tano lakini golikipa Mwadini Ally alifanikiwa kuucheza mpira huo.


Erasto Nyoni awe ‘ busy’ kumkimbiza uwanjani, huku Danny Sserunkuma akifanya hivyo kwa Shomari Kapombe. Mashambulizi mfululizo yalizaa ‘ bao la video’ lililofungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 19. Okwi alimchungulia kwa mbali Mwadini kabla ya kuupiga mpira kiufundi na kufunga bao lake la nne msimu huu.
Baada ya kufungwa goli hilo la ‘ mbinu na ufundi’, wachezaji wa Azam walianza kucheza mchezo wa nguvu. Na ndani ya dakika 10 kipa wa Simba, Manyika Peter alikuwa ‘ busy’ kuokoa ‘ michomo’ ya Didier Kavumbagu na Kipre. Kama angekuwa makini, ‘ Kavu’ angeweza kufunga goli la kusawazisha kufuatia pasi ‘ murua’ ya Kipre katika dakika ya 33. Akiwa karibu kabisa la lango, Mrundi huyo alipaisha mpira baada kutumia nguvu nyingi kuupiga mpira huo. Ilikuwa ni nafasi ya wazi zaidi ambayo Azam waliitengeneza na ukosefu wa umakini ukawasaidia Simba kuendelea kuongoza mchezo.
Tatizo la washambuliaji kukosa umakini lilikuwepo hata upande wa Simba. Simba wakiwa mbele kwa bao 1-0, mshambulizi Elius Maguli alipumzishwa mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na nafasi yake ikachukiliwa na Simon Sserunkuma. Mabadiliko hayo yaliyofanywa na kocha, Goran Kopunovic mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili yaliifanya timu kudili mfumo wake wa kiuchezaji kutoka 4-4-2 hadi 4-3-3 ili kujaribu kupunguza nguvu ya Azam FC katikati ya uwanja.
Maguli, Danny, Okwi na Singano hawakuwa wakikaba sana na hivyo kuwapa wakati mgumu Jonas Mkude na Said Ndemla ambao kadri muda ulivyokuwa ukisogea walionekana kuzidiwa na viungo, Frank Domayo, Himid Mao, Kipre Bolou na Mudathir Yahya. Azam walikuwa na stamina zaidi, labda ndiyo sababu ya mchezo huo kuonekana wa uabe mwingi lakini ndivyo ilivyo hasa katika michezo mikubwa kama hii.
Kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, kocha wa Azam, Joseph Omog aliamua kumpumzisha Domayo mara baada ya Simba kufanya mabadiliko ya kwanza. Hamis Mcha aliingia ili kwnda kuichezesha timu na kuiongezea ufanisi na kasi katika safu ya mashambulizi. Baada ya kuingia kwa Mcha, Azam ilionekena kucheza katika mfumo wa 4-3-3 na kuachana na ule wa 4-4-2 walioutumia kipindi cha kwanza ili kusawazisha, na walikuja kufanikiwa katika hilo baada ya Simba kuchoka.
Kuingia kwa John Bocco dakika ya 54 ili kumbadili, ‘ Kavu’ aliyepoteza nafasi nyingi ilikuwa ni sawa na kulazimisha kufun ga mbele ya safu ya ulinzi ‘ ambayo haikufanya makosa mengi’. Kipre alifunga bao zuri la ‘ kiki’ dakika ya 57 na baada ya bao hilo mechi ilikuwa na ‘ ubabe mwingi’. Mcha, Himid, Kessy walipata kadi za njano. Ilikuwa ni mechi ya kipa chipukizi Manyika Jr baada ya kucheza mipira mingi ya hatari dakika kumi za mwisho.
Kitendo cha kusawazisha inaonesha wazi kuwa kikosi cha Azam kimeendelea kuimarika hasa ukizingatia timu ya Mtibwa Sugar imepoeza mbele ya Ruvu Shooting kwa kulazwa mabao 2-1. Ligi imekuwa ngumu kweli kweli, na nafikiri mashabiki wa klabu kubwa watakuwa na majibu ya kutosha hivi sasa kwani timu zimekuwa na mbinu bora. Nilkipenda namna Azam walivyokuwa wakizuia na kushambulia. Ukabaji wao katika idara ya kiungo ulikuwa ni wa kiwango cha juu, kwani licha ya Simba kumiliki mpira wakati Fulani hawakufanikiwa kutengeneza nafasi za hatari. Soka limetenda haki,

Post a Comment

 
Top