Mfanyabiashara maarufu nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusufu Manji amepata dhamana baada ya kusomewa shtaka moja la kutumia dawa za kulevya aina ya heroine.
Manji amesomewa shtaka hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya wakili wake Alex Mgongolwa kuiomba dhamana na Jamhuri kusema haina pingamizi kwani shtaka hilo linadhaminika.
Hakimu Cyprian Mkeha amesema Manji atakuwa nje kwa dhamana kwa sharti la kusaini bondi ya dhamana ya Sh 10 milioni na awe na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya Sh 10 milioni.
Amedhaminiwa na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwassa.
Post a Comment