Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez leo asubuhi ameonekana katika uwanja wa ndege wa Heathrow akipanda pipa kwenda mapumzikoni ambapo hapakujulikana baada ya kipigo kikali cha mabao 5-1 kwa timu yake kutoka kwa Klabu ya Bayern Munich jana usiku.
Sanchez aliyekuwa amaevalia mavazi meusi ameonekana akiwa mnyonge na amechoka wakati akiwa uwanjani hapo tayari kwa safari huku mkononi akiwa na passport yake.
Imeelezwa kuwa huenda staa huyo akaukosa mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Sutton United.
Sanchez alifanikiwa kuifungia timu yake bao la kufutia machozi katika mechi hiyo ya 16 Bora ya Michuano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya iliyopigwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Bayern Munich, Allianz Arena.
Post a Comment