0

Kuna kila dalili Yanga itabaki jijini Dar es Salaam na kucheza na kikosi cha MC Alger kutoka Algeria.

Awali Yanga ilitaka kucheza mechi yake hiyo mjini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, mechi ambayo imepangwa kucheza Aprili 8.

Lakini masharti ya kufanya ukarabati, kuweka ofisi ndogo ya Caf na kadhalika, inaonekana kuifanya Yanga ibaki Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa naye amesema ni kama asilimia miaka wanaweza kuendelea kubaki.

“Nafikiri tutabaki, siwezi kusema tunawakimbia Mwanza lakini kuna mambo mengi yamejitokeza katikati.

“Kikubwa ni kwamba kuna mambo mengi ya ukarabati katika uwanja wa CCM Kirumba na hayajakamilika. Tutabaki Dar es Salaam na ikitokea siku nyingine, tunaweza kwenda Mwanza au kwingine kokote ambako tunajua Wanayanga wanastahili kuiona timu yao,” alisema.

Post a Comment

 
Top