Klabu ya Manchester City imepata idhini ya kumnunua rasmi winga wa Brazil mwenye umri wa miaka 19, Gabriel Jesus na sasa anaweza akacheza dhidi ya Tottenham Jumamosi.
Jesus amehamia City kutoka klabu ya Palmeiras ya Brazil kwa £27m.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alikubali kuhamia City kwa mkataba wa miaka mitano Agosti mwaka jana ila aliendelea kuwa na Palmeiras hadi mwisho wa msimu wa soka Brazil mwezi Desemba.
"Ana uwezo wa kuibuka kuwa miongoni mwa washambuliaji bora zaidi katika soka," Mkurugenzi wa soka wa City, Txiki Begiristain alisema.
Jesus alifika City mwanzoni mwa mwezi huu lakini alichelewa kupata idhini ya kusajiliwa City, taarifa zikisema Shirikisho la Soka la Uingereza lilikuwa linachunguza stakabadhi kuhusu uhamisho wake.
City wanamchukulia mchezaji huyo kuwa chipukizi mwenye kipaji zaidi Amerika Kusini kwa sasa, na waliwapiku Barcelona kumchukua.
Jesus amesema meneja wa City, Pep Guardiola alichangia sana katika uamuzi wake wa kuhamia klabu hiyo.
Post a Comment