Kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.
Na Sweetbert Lukonge, ZanzibarKIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mbrazili, Andrey Coutinho amemsababishia balaa kocha mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, visiwani hapa na kufanya ajiulize maswali mengi bila ya kuwa na majibu.
Mashabiki wa Yanga wanaofika katika Uwanja wa Amaan kwa ajili ya kuiunga mkono timu hiyo, wamekuwa wakisema wanamkubali sana, ila wana wasiwasi na viongozi wa timu hiyo kuwa wanaweza kumtema.
Wakizungumza na Kocha Mkuu wa Yanga, mashabiki hao walisema wana hofu kubwa kuwa anaweza kupigwa majungu na viongozi waliopo. “Tunampenda sana Coutinho, ndiyo maana kila mtu anamzungumzia yeye ni mmoja kati ya wachezaji wazuri wa klabu yetu.
“Ila hofu yetu kubwa ni kwamba anaweza akaondoka kabla ya kutufanyia kazi tunayotaka kwa sababu ya chuki za viongozi, hivyo tunakuomba uliangalie hilo kwa umakini mkubwa.
“Sisi tunawajua sana hawa viongozi wetu walivyo,” walisema mashabiki hao.
Hata hivyo, Pluijm aliowaondoa wasiwasi kwa kuwaambia kuwa “Nitalifanyia kazi jambo hilo.”
Coutinho ni Mbrazili pekee aliyebaki hapa nchini baada ya Marcio Maximo na msaidizi wake kutupiwa virago hivi karibuni ingawa awali alianza kuondoka Geilson Santana ‘Jaja’.
Post a Comment