Na Ibrahim Mussa
BEKI mpya wa
Simba, Hassan Kessy, ameuomba radhi uongozi wa Mtibwa kutokana na rafu
mbaya aliyomchezea, Ibrahim Rajabu ‘Jeba’ katika mchezo wa Kombe la
Mapinduzi uliozikutanisha timu hizo hivi karibuni.
Beki huyo kabla ya kutua Simba alikuwa akiichezea Mtibwa, baada ya
kutokea tukio hilo viongozi wa Mtibwa walikuja juu na kumshutumu
kutokana na kitendo hicho ambacho si cha kiungwana.
Akizungumza Kessy alisema rafu ile ni bahati
mbaya na kwenye mchezo inatokea, lakini anaomba asamehewe kwa kitendo
kile kwani hana ugomvi na mchezaji huyo.
“Nimeondoka Mtibwa kwa amani na wala sijawahi kuwa na ugomvi kuanzia
kwa viongozi mpaka kwa wachezaji kwa sababu mpaka naondoka kila kitu
kilikuwa sawa.
“Unajua sikupanga kumchezea rafu Jeba kama inavyotafsiriwa, lakini
imetokea bahati mbaya kama sehemu ya mchezo na tunapaswa kusameheana,
sasa nafanya kazi pamoja na Simba, hivyo ninahitaji Baraka zao ili
nijitume na kufanikiwa,” alisema Kessy.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment