Na Sweetbert Lukonge, Zanzibar
KOCHA
Mkuu wa Simba, raia wa Serbia, Goran Kopunovic, amewashangaa viongozi
wa klabu hiyo kwa kumuacha Amissi Tambwe kwenye usajili uliopita.Simba
waliachana na Tambwe kwenye usajili uliopita kwa kile walichodai kuwa,
ameshuka kiwango pamoja na kwamba msimu mmoja tu nyuma aliwapa heshima
ya kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Tambwe baada ya kuachwa, alijiunga na Yanga ambayo mpaka sasa
ameshaifungia bao moja kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara walipocheza dhidi
ya Azam.Akizungumza na Championi Jumatano, Kopunovic ambaye amejiunga na
Simba baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Patrick Phiri
kutupiwa virago, alisema ameshangaa sana kusikia kuwa mshambuliaji huyo
aliachwa na Simba, kwani anaonyesha kiwango kizuri sana.
Jumapili iliyopita, Kopunovic aliyetua Simba hivi karibuni kuchukua
mikoba ya Patrick Phiri aliyetimuliwa klabuni hapo, alipigwa na butwaa
baada ya kuambiwa kuwa Tambwe alikuwa mchezaji wao ila uongozi wa timu
hiyo ulimfungashia virago kwa madai kuwa ameshuka kiwango.
“Nimemuona ni mchezaji mzuri sana, anaonekana anajua kufunga na kuisaidia timu yake.
“Lakini
nashangaa kusikia kuwa alikuwa Simba akaachwa, ndiyo hivyo tena
imeshatokea lakini naamini hata wachezaji wangu ni wazuri kama yeye,”
alisema kocha huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment