Sweetbert Lukonge na Kazija Thabit, Zanzibar
NI
sahihi kusema kuwa Mzungu halogeki baada ya Yanga kumaliza mechi yake ya
mwisho ya makundi jana dhidi ya Shaba kwa ushindi mzuri wa bao 1-0.
Katika mchezo huo wa Kombe la Mapinduzi ulipigwa kwenye Uwanja wa
Amaan, ulikuwa na vituko vya hapa na pale baada ya shabiki mmoja wa
Yanga kuamua kujitoa mhanga na kuingia uwanjani kwenda kuzoa glovu za
kipa kwa imani kuwa zinazuia mpira usiingie wavuni.
Hiyo ilitokea baada ya Yanga kukosa zaidi ya mabao nane ya wazi na
dakika tatu tu baada ya glovu hizo kutolewa, Mbrazili Andrey Coutinho,
akaifungia Yanga bao pekee katika dakika ya 86 na mashabiki kuanza
kuimba ‘Mzungu halogeki’.
Hilo ni bao la tatu kwa Mbrazili huyo kwenye michuano hiyo na
anashika nafasi ya pili kwa wafungaji wa timu hiyo nyuma ya Simon Msuva
ambaye ana mabao manne.Kuingia kwa Amiss Tambwe na Kpah Sherman katika
kipindi cha pili kuliongeza nguvu kwa Yanga na kusababisha kupatikana
kwa bao hilo.
Yanga ndiyo watamu zaidi kama tangazo maarufu sana kwa sasa
linalosema ‘Mcharo kwenye michuano hiuo baada ya kuwa timu pekee
kumaliza kwenye hatua ya makundi kwa kishindo baada ya kushinda michezo
yake yote mitatu.
Katika michezo hiyo Yanga wamekusanya pointi tisa na mabao tisa,
baada ya kushinda 4-0 kwenye michezo miwili mfululizo ya kwanza.Yanga
haijaruhusu lango lake kutikiswa kwenye michuano hiyo katika michezo
yote na sasa watavaana na JKU Kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali
kesho.
Hata hivyo, kiwango cha timu hiyo kinatisha amani kwani kama
watakutana na timu dhaifu wanaweza kuifunga hata mabao tisa kutokana na
kiwango cha juu walichoonyesha.
Huku washambuliaji wake wakiwa na uchu wa hali ya juu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment