Na Khadija Mngwai
BAADA ya
kiungo wa Yanga, Andrey Coutinho, raia wa Brazil, kufanikiwa kufumania
nyavu mara mbili katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Polisi
Zanzibar, kocha mkuu wa timu hiyo, Hans van Der Pluijm, amefunguka kuwa
kiwango cha mchezaji huyo kipo juu kwa sasa.
Pluijm alianza kwa kumuweka benchi kiungo huyo kwenye mchezo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam, lakini michuano ya Kombe la Mapinduzi
imemuamsha.Coutinho alifanikiwa kuifungia timu yake mabao mawili kati ya
manne waliyofunga katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Polisi
Zanzibar.
Akizungumza na Championi Jumatano, Pluijm amefunguka kuwa
amefurahishwa na uwezo unaoonyeshwa na Mbrazili huyo kwani amekuwa
akibadilika kila siku.“Coutinho ni mchezaji mzuri na amekuwa akielewa
vyema maelekezo yangu.
“Hakika kwa sasa anaonyesha kiwango kizuri sana uwanjani na kila siku amekuwa akionyesha mabadiliko makubwa,” alisema Pluijm.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment