Na Sweetbert Lukonge, Zanzibar
UWEZO
wa hali ya juu unaonyeshwa na safu ya ushambuliaji ya Yanga umempa
kiwewe Kocha wa Simba, Goran Kopunovic na kujikuta akisema hawa jamaa ni
noma.
Mserbia huyo wa Simba aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni
akichukua mikoba ya Mzambia, Patrick Phiri, amesema kuwa washambuliaji
hao ni hatari na ni watu wa kuchungwa sana katika mashindano haya.
Ijumaa
iliyopita washambuliaji wa Yanga, Simon Msuva na Kpah Sherman
walionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo, huku Msuva akifunga moja
na Sherman moja.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kopunovic alisema tangu ameanza
kufuatilia mashindano hayo, Yanga ndiyo wana washambuliaji bora zaidi.
“Nimejifunza mambo mengi katika mashindano haya na ninaendelea kujifunza
ili niweze kuona tofauti iliyopo kati ya timu yangu na nyingine
zinazoshiriki michuano hii.
“Hata hivyo kuna mambo ambayo tayari nimeshayaona na nitakuwa
nikiyafanyia kazi kidogo kidogo ili kikosi changu kiweze kuwa bora
zaidi, ninaamini nitafanikiwa juu ya hilo.
“Safu hatari ya ushambuliaji ambayo mpaka sasa imenivutia ni ile ya
Yanga, hususani wachezaji wale waliofunga mabao dhidi ya Jang’ombe
(Msuva na Sherman) jamaa ni hatari,” alisema Kopunovic ambaye pia juzi
Jumamosi aliongoza timu yake kupata ushindi wake wa kwanza katika
mashindano haya dhidi ya Mafunzo baada ya kushinda bao 1-0.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment