Na Sweetbert Lukonge, Zanzibar
SIKU
chache baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia, Goran Kopunovic kufanya
mkutano wa siri na wachezaji wa timu hiyo kisiwani hapa amemtaka kocha
msaidizi, Selemani Matola kumkabidhi majina ya wachezaji wasumbufu.
Kutokana na hali hiyo kwa namna moja ama nyingine jina la
mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi pamoja na Waganda wenzake,
Simon Sserunkuma, Juuko Murushid na Joseph Owino lazima majina yao
yafike mikono kwa Mzungu huyo.
Hivi karibuni Okwi pamoja na wenzake walimkera Matola kutokana na
kitendo chao cha kushindwa kujiunga na timu hiyo kwa wakati kwa ajili ya
kushiriki Kombe la Mapinduzi linaloendelea kutimua vumbi visiwani hapa.
Matola aliwatuhumu wachezaji hao kuwa kukosekana kwao kuliifanya timu
hiyo ipoteze mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar kwa bao
1-0.Akizungumza na Championi Jumatatu, Kopunovic alisema kuwa amempatia
Matola kazi hiyo ili aweze kupambana nao kwa faida ya timu.
Alisema ili Simba iweze kufanya vizuri katika michuano hii na Ligi
Kuu Bara, wachezaji wote wanatakiwa kuwa kitu kimoja.“Nidhamu ni jambo
muhimu kwa kila mtu hapa duniani, huwezi kuwa na mafanikio kama huna
nidhamu, hivyo ili Simba iweze kufanya vizuri inabidi kulisimamia hili.
“Sitamvumilia mchezaji yeyote atakayefanya mambo yake kinyume na
utaratibu wetu, ndiyo maana nimemtaka Matola anipatie majina ya
wachezaji wasumbufu ili nijue nitafanyaje kuhakikisha wanakuwa sawa,”
alisema Kopunovic.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment