Aliyekuwa kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal amesema kuwa hajastaafu kufundisha soka na kwamba anachukua likizo ya muda.
Van Gaal mwenye umri wa miaka 65 hajajiunga na timu yoyote tangu aondoke Old Trafford mwezi Mei.
Juzi Jumatatu, gazeti moja la Uholanzi, De Telegraaf lilisema Van Gaal amemaliza muda wake wa ukufunzi na amestaafu kama mkufunzi, hatua ilioshinikizwa na kifo cha mwanawe.
Lakini Gaal alikiambia kituo kimoja cha redio nchini Uhispania, Cadena Ser kwamba japokuwa kustaafu kunawezekana lakini bado hajaamua.
Raia huyo wa Uholanzi pia alifunguka kuwa amekataa kuifunza klabu ya Hispania, Valencia mwezi uliopita.
"Iwapo nitaendelea au la pia itategemea na maombi nitakayopata, aliongezea.
"Nimevifunza vilabu vingi na nadhani ni vigumu kuviinua vikiwa katika hali hiyo.
Siyo kweli kwamba nimestaafu, siyo sasa, lakini nitaamua mwisho wa likizo yangu mwezi Juni ama Julai."
Post a Comment