0







KLABU ya Southampton imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool katika mechi yao ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Ligi (EFL Cup) iliyochezwa jana usiku.

Bao pekee la Southampton waliokuwa nyumbani liliwekwa kimiani na Nathan Redmond katika dakika ya 20 ya mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa St Mary's.

Timu hizo zitarudiana Januari 25, 2017 katika Uwanja wa Anfield, Liverpool ambapo mshindi atachuana na mshindi kati ya Manchester United na Hull City kwenye fainali itakayopigwa Februari 26, 2017.

Post a Comment

 
Top