Simba Nao Mzigoni Kuhakikisha Wanamzima Lambalamba Hapo Kesho
Kikosi cha timu ya Simba SC asubuhi ya leo kimefanya mazoezi huko Visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wake wa fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC.
Simba SC ambao wametinga hatua hiyo ya fainali kwa kuwachapa watani wao wa jadi Yanga SC kwa penalti 4-2 watakuwa na kibarua cha kuwazuia Azam FC waliotinga kwenye fainali hizo kwa kuichabanga bao 1-0 timu ya Taifa Jang'ombe.
Mechi hiyo ya fainali inayosubiriwa kwa hamu na mamilioni ya wapenzi wa soka itapigwa saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar
Post a Comment