0


Staa aliyewahi kuzichezea klabu za Chelsea na Real Madrid, Claude Makelele (pichani juu) amekula shavu baada ya kuteuliwa kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Swansea inayoshiriki Ligi Kuu ya England.

Makelele kwa sasa atakuwa msaidizi wa Meneja Paul Clement ambaye tayari walishafanya naye kazi akiwa Chelsea wakati Makelele akiwa mchezaji na baadaye wakakutana tena kwenye benchi la klabu ya PSG wakiwa chini ya kocha Carlo Ancelotti.


Pichani juu Paul Clement akiwa na Makelele wakati wapo PSG.
Makelele (43) amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa msimu.

CV YA MAKELELE

PLAYING
1991–97 Nantes
1997–98 Marseille
1998–00 Celta Vigo
2000-03 Real Madrid
2003–08 Chelsea
2008–11 PSG

HONOURS
Ligue 1, La Liga (x2), Champions League, Super Cup, Premier League (x2), League Cup (x2), FA Cup

1995–08 France 71 caps (0 goals)

COACHING
2011-13 PSG (assistant)
2014 Bastia
2016 Monaco (coach)
2017- Swansea (assistant)

Post a Comment

 
Top