0



MTANGAZAJI wa Kipindi cha Amplifaya kinachoruka kupitia Clouds Radio, Millard Ayo amechaguliwa kuwa mmoja wa watangazaji watakaoripoti mechi za michuano ya AFCON 2017 kutoka uwanjani nchini Gabon.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Ayo ameandika haya; "Ni good news kwangu kwa kweli, nimechaguliwa na shirikisho la soka Afrika ktk list ya Waandishi wataoripoti michuano ya Afrika toka uwanjani".

Michuano hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi Jumapili ya Januari 15, 2017 huko nchini Gabon.

Tunamtakia kila la heri Millard Ayo.

Post a Comment

 
Top