Nahodha wa Azam FC, John Bocco na beki wa Simba SC, Besala Jenvier Bukungu wametambiana kila mmoja akiipa nafasi kubwa timu yake kuibuka na ubingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi kwenye fainali inayopigwa leo saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Bocco amesema wao wamejiandaa vizuri na wana morali kubwa ya kuibuka na ushindi na watatoa ushindani mkubwa kwa wapinzani wao Simba na kuandika historia nyingine.
Bocco. |
"Simba ni timu nzuri tangu wanaanza michuano hii na sisi tunalifahamu hilo ila tumejipanga vizuri kuweza kuibuka na ushindi kwenye fainali ya leo na kuweka historia." Amesema Bocco
Naye beki wa Simba aliyepiga penalti ya mwisho dhidi ya watani wao Yanga, Besala Jenvier Bukungu amesema nao wamejipanga vyema na kuwaomba mashabiki wafike kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao ya Simba.
Bukungu. |
"Tunashukuru kwanza kwa kufika fainali, na tunawaomba mashabiki wetu wafike kwa wingi, Azam ni timu kubwa na Simba pia ni timu kubwa, lakini mashabiki wetu watafurahi baada ya mechi ya leo." amesema Bukungu
Post a Comment