Nahodha wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa "Fuso" ambaye alikuwa nahodha wakati Godfrey Bonny "Ndanje" akiichezea Yanga amesema marehemu Ndanje alikuwa mchezaji mahiri sana uwanjani akiwa na ushirikiano mkubwa na wenzake.
Aidha Nsajigwa amesema anachokikumbuka sana kwa Ndanje ni wakati wakiichezea timu ya taifa, Taifa Stars ilipokutana na Cameroon ambapo Bonny alionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwafanya mashabiki wa soka wamjue vizuri kiungo huyo.
Nsajigwa. |
Bonny maarufu kama Ndanje amefariki dunia baada ya kulazwa kwa muda mrefu katika Hospitali ya Makandana iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya.
Kiungo huyo aliichezea Yanga kwa kiwango kikubwa akitokea Tanzania Prisons ya jijini Mbeya. na baada ya kuachana na Yanga alikwenda kucheza soka la kulipwa nchini Nepal.
Post a Comment