0


Hatimaye kocha wa Klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anajiandaa kuachana na timu hiyo baada ya kuiongoza kwa miaka 21.

Wenger anatarajia kufanya maamuzi hayo mwishoni mwa msimu huu.

Akinukuliwa baada ya mechi ya hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya juzi dhidi ya Bayern Munich iliyomalizika kwa Arsenal kulala kwa mabao 5-1, Wenger alisema kwamba hatima yake na Arsenal itajulikana kati ya mwezi Machi au Aprili.
Kocha wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo kelele nyingi kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo wakimtaka kocha huyo kuondoka baada ya kushindwa kuchukua makombe.

Baadhi ya wanahisa wa klabu hiyo akiwemo Stan Kroenke wanataka Wenger aendelee kukinoa kikosi hicho cha jijini London. 

Baadhi ya viongozi wa ngaji za juu wa klabu hiyo wanadhani kocha wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino anaweza kuvaa viatu vya Wenger kwa kukinoa kikosi hicho iwapo Wenger ataondoka.

Post a Comment

 
Top