0


UONGOZI wa Yanga umesema kwamba hauna mpango wa kumfukuza kocha wake, Mzambia George Lwandamina baada ya timu yao kutolewa kwenye Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.

  
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana, Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema kwamba uongozi unaridhishwa na kazi ya Lwandamina hadi sasa licha ya timu kutolewa katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi.

“Tunashangazwa na taarifa za kizushi kwamba Lwandamina anafukuzwa, afukuzwe kwa sababu gani. Hakuna kitu kama hicho. Lwandamina bado yupo, na ataendelea kuwapo,” alisema Baraka.


Uvumi wa kwamba Lwandamina anafukuzwa kazi Yanga ulianza kuzagaa juzi baada ya timu hiyo kutolewa na mahasimu wao Simba SC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 baada ya dakika 90. 

Post a Comment

 
Top