0


ZIKIWA zimesalia saa chache kuelekea pambano la fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kati ya Simba SC na Azam FC katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar presha ya mechi hiyo inaonekana kuwa kubwa huku kila timu ikiwa na nafasi kubwa ya kulitwaa kombe hilo.

Upande wa Azam ambao mpaka wanatinga hatua ya fainali hawajaruhusu hata bao moja langoni mwao wakianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimamoto kisha wakatoka suluhu na Jamhuri kabla ya kuifumua Yanga mabao 4-0, kisha kutinga fainali baada ya kuipa kichapo cha bao 1-0 Taifa Jang’ombe.

Wekundu wa Msimbazi wao wametinga fainali wakiwa wameruhusu bao moja pekee katika dakika 90 za michezo yake iliyocheza katika michuano hii ya Mapinduzi.

Walianza kwa ushindi wa bao 2-1 dhid ya Taifa Jang'ombe, kisha wakaichapa KVZ bao 1-0 na kutoka suluhu na URA kabla ya kuichapa Jang'ombe Boys bao 2-0 na kukutana na watani wao Yanga katika nusu fainali na kuiondoa kwa penalti 4-2 baada ya suluhu kwenye muda wa kawaida.

Kwa rekodi hizo inaonyesha ni jinsi gani mechi ya leo itakavyokuwa kali kutokana na timu hizo kuwa vizuri katika kila idara.

Iwapo Simba watashinda kwenye fainali hii watakuwa wamelitwaa mara nne Kombe la Mapinduzi na iwapo Azam ndiyo watashinda watakuwa wamelitwaa kwa mara ya tatu sawa na Simba.

Post a Comment

 
Top