KLABU ya Arsenal imewaongeza mikataba wachezaji wake watatu Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francis Coquelin huku ikijiandaa kuwaongezea na majembe wake wengine wawili Mesut Ozil na Alexis Sanchez.
Zoezi hilo limeongozwa na kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger ambapo Laurent Koscielny amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu mpaka mwaka 2020 huku Giroud akisaini mkataba wa miaka miwili na nusu wakati Coquelin akijipiga pini kwa miaka minne na nusu.
Mishahara yao kwa wiki itakuwa kama ifuatavyo; Coquelin £75,000, Giroud £90,000 na Koscielny £80,000.
Post a Comment