0


MASHABIKI wa soka mkoani Pwani kesho wanatarajia kushuhudia 'derby' kati ya timu za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ruvu Stars na Ruvu Shooting zinazotarajiwa kumenyana kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
JKT Ruvu.

Kufuatia mtanange huo, Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire amejinadi kuwa timu yake itaibuka kidedea kutokana na historia ya timu hizo zinapokutana.
Ruvu Shooting.

"Kiukweli mechi itakuwa na ushindani hapo kesho lakini kutokana na historia na jinsi vijana wangu walivyoandaliwa kisaikolojia na mwalimu, lazima tuibuke na ushindi kwenye mchezo huo dhidi ya wenzetu wa JKT Ruvu." Amesema Bwire

Post a Comment

 
Top