0




Staa wa timu ya taifa ya England na klabu ya Arsenal, mwanamama Kelly Smith ametangaza rasmi kustaafu soka la kulipwa akiwa na miaka 38.

Staa huyo mwenye rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa England akiwa amezama kambani mara 46, ndiye Mwingereza wa kwanza kucheza soka la kulipwa alipojiunga na timu ya New Jersey mwaka 1999.

Mama huyo amejishindia vikombe 117 akiwa na England huku akishiriki katika michuano mikubwa sita na kuiwakilisha timu ya Uingereza kwenye michuano ya Olimpiki mwaka 2012.


Smith amejishindia pia makombe matano ya FA akiwa na klabu yake ya Arsenal, huku akitupia kambani mabao sita katika fainali hizo.


"Naona muda sahihi ndiyo huu sasa

"Nahisi nimekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi cha uchezaji wangu kwenye timu ya taifa pamoja na klabu yangu, Nimesafiri duniani na katika umri huu wa miaka 38, mwili wangu unaniambia unahitaji kupumzika

"Sina cha kujutia chochote, nimekuwa nikifurahia kila dakika wakati wa uchezaji wangu, kila nivaapo jezi ya timu yangu ya England najihisi morali kubwa kuichezea nchi yangu." Ameeleza staa huyo.

Post a Comment

 
Top