STAA wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani, Mesut Ozil ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2016 nchini Ujerumani.
Staa huyo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya tano sasa baada ya kuishinda mwaka 2011, 2012, 2013, 2015 na 2016.
Ozil mwenye umri wa miaka 28, alipata asilimia 54.5 ya kura zote zilizopigwa 316,850 huku, staa wa Real Madrid Toni Kroos akishika nafasi ya pili baada ya kupata asilimia 33.9 za kura.
Akiongea kupitia tovuti ya timu ya taifa ya Ujerumani baada ya ushindi wa tuzo hiyo, Ozil alisema;
'Nimebadili vitu vichache katika maisha yangu kwenye mwaka huu uliopita, kwa mfano mlo wangu na mazoezi.
Vitu hivyo vimenisaidia kuwa mwepesi uwanjani na kunipunguzia uwezekano wa kupata majeraha.'
2011: 🏆— Germany (@DFB_Team_EN) January 15, 2017
2012: 🏆
2013: 🏆
2015: 🏆
2016: 🏆
Congrats on winning #DieMannschaft's Player of the Year award again, @MesutOzil1088! pic.twitter.com/WgjfW40nXn
Post a Comment