KIKOSI cha Ivory Coast kikiwa na mastaa wake akiwemo Eric Bailly katika nafasi ya beki, Franck Kessie nafasi ya kiungo, Wilfried Zaha kwenye safu ya ushambuliaji na Jonathan Kodjia huku Wilfried Bony akiingia kipindi cha pili bado imeshindwa kuwazuia Togo na kulazimishwa suluhu katika mechi yao ya kwanza ya michuano ya AFCON 2017 kutoka Kundi C.
Mastaa hao walishindwa kufurukuta kwa Togo iliyokuwa ikiongozwa na mshambiliaji asiyekuwa na klabu kwa sasa Emmanuel Adebayor, Serge Gakpe akiwa nafasi ya beki na kiungo akiwepo Floyd Ayite.
Post a Comment