0


BAO la Junior Kabananga limeipatia ushindi wa pointi tatu timu ya taifa ya DR Congo dhidi ya Morocco kwenye mchezo wao uliopigwa usiku huu kutoka Kundi C katika michuano ya AFCON 2017 inayoendelea nchini Gabon.


Kabananga ameipatia timu yake bao dakika ya 55 mbali na kwamba Morocco waliutawala mchezo huo.

Kwa ushindi huo, DR Congo ndiyo vinara wa Kundi C wakiwa na pointi tatu huku Ivory Coast na Togo zikifuatia kila moja ikiwa na pointi moja na mkiani wapo Morocco wasio na pointi.



Post a Comment

 
Top