0


MCHEZAJI wa zamani wa Barcelona ambaye kwa sasa ni Kocha wa klabu ya Everton, Ronald Koeman amempongeza Lionel Messi (pichani chini) baada ya kufikia rekodi yake ya kufunga mabao 26 ya 'free kick' kwa timu ya Barcelona jana usiku.

Messi alifunga bao lake la 26 la 'free kick' na kuipelekea timu yake ya Barcelona katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa del Rey wakiitupa nje Athletic Bilbao.

Baada ya ushindi huo, bosi wa Everton (pichani chini) aliyeichezea Barcelona kuanzia mwaka 1989 hadi 1995 akiifungia jumla ya mabao 67 kwa mechi 192 alizocheza, alimpongeza Messi kupitia akaunti yake ya Instagram amabapo aliandika: 'Hongera kwa kufunga bao lako la 26 kwa free kick @fcbarcelona tonight, @leomessi! bado bao moja kuvunja rekodi nyingine.'
Katika mchezo huo, Luis Suarez aliifungia klabu yake hiyo bao la 100 tangu ajiunge na wakali hao wa Hispania.

Post a Comment

 
Top