0


KIUNGO wa Everton, Tom Cleverley (pichani juu) anatarajia kujiunga na klabu ya Watford leo kwa mkopo baada ya klabu hizo mbili kukubaliana.

Kiungo huyo alikuwa anawaniwa pia na vilabu vya Newcastle United, Burnley na Aston Villa.

Cleverley amekuwa akipigania kupata namba klabuni hapo chini ya kocha Ronald Koeman lakini hatua ya Everton kumsajili kiungo wa kati Morgan Schneiderlin kutoka Man United inapunguza nafasi ya staa huyo kuendelea kuwepo kwenye kikosi hicho.

Everton wapo mbioni pia kumnasa kiungo wa Atalanta, Franck Kessie pamoja na straika kutoka Standard Liege, Ishak Belfodil.

Post a Comment

 
Top