Takwimu zinaonesha kuwa katika mechi 4 ambazo watani wa jadi Simba na Yanga wamekutana visiwani Zanzibar, Simba imeshinda mechi 3 huku Yanga ikishinda mechi 1 pekee, jambo ambalo linampa imani Msemaji wa Simba, Haji Manara ambaye amesema Simba ni lazima ishinde kutokana na kuwa na kikosi bora kuliko Yanga.
Kwa upande wa Yanga, wapenzi na mashabiki zake wametoa tambo kuwa ni lazima mnyama achinjwe kwa kuwa Simba haina kitu, na haina kikosi imara kama cha timu yao, huku wakijipa moyo kuwa kufungwa na Azam ilikuwa ni njia ya kutafuta hasira za kumuangamiza mnyama na wala hakuwastui.
Mchezo wa mwisho kwa timu hizo kukutana Zanzibar, Simba ilishinda mabao 2-0 kupitia kwa Musa Mgosi na Shija Mkina. (Pichani juu ni sehemu ya mechi hiyo)
Post a Comment