Habari Njema Kutoka FIFA, Sasa Kombe la Dunia Kuwa na Timu 48
Shirikisho la Soka Duniani FIFA limepitisha mabadiliko ambapo kuanzia mwaka 2016 timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia zitaongezeka kutoka 32 hadi 48.
Mpango huo umepitishwa leo katika mkutano wake mkuu nchini Uswizi kwa kupigia kura mpango wa kupanua Kombe la Dunia liwe linashirikisha mataifa 48 huku mabara ya Afrika na Asia yakitarajia kunufaika zaidi.
Kupitia mabadiliko hayo, kuanzia katika mashindano ya mwaka 2026, kutakuwa na makundi matatu yenye timu 16 kila moja.
Mpango huo umekuwa ukipigiwa debe na Rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino.
Post a Comment