KLABU ya Arsenal imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja beki wake ambaye ni raia wa Ujerumani, Per Mertesacker.
Beki huyo ambaye amekuwa benchi kutokana na majeraha anatarajia kurejea kikosini hivi karibuni baada ya afya yake kuzidi kuimarika.
Mbali na kuwa timu hiyo inao mabeki wengine kama Shkodran Mustafi na Laurent Koscielny, kocha wake Arsene Wenger amesema kuwa kutokana na mechi zinazoikabili timu yake, ni muhimu kuwa na wachezaji wao wote wenye uzoefu hasa katika nafasi ya ulinzi.
Post a Comment