MABINGWA mara nne wa michuano ya AFCON, Cameroon usiku huu wamefanikiwa kukaa kileleni mwa Kundi A baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Guinea-Bissau.
Guinea-Bissau ndiyo walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 13 kupitia kwa Brito Silva huku Cameroon wakisawazisha dakika ya 61 kupitia kwa Sebastien Siani na baadaye kuongeza bao la pili katika dakika ya 78 kupitia kwa Michael Ngadeu-Ngadjui.
Kwa ushindi huo, Cameroon wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi 4, wakifuatiwa na Gabon na Burkina Faso wenye pointi 2 kila mmoja huku Guinea-Bissau akishika mkia akiwa na pointi moja.
Post a Comment