TIMU ya Azam FC itamenyana na Taifa Jang’ombe katika Nusu Fainali ya kwanza Kombe la Mapinduzi kesho Jumanne saa 10:15 jioni kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hiyo inafuatia Taifa kuwalaza waliokuwa mabingwa watetezi, URA ya Uganda 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi A uliopigwa jana usiku ndani ya Uwanja wa Amaan.
Bao pekee la Taifa Jang’ombe lilifungwa na Mohammed Said kwa penalti, baada ya Ally Badru kuangushwa kwenye boksi.
Nusu fainali ya pili itaikutanisha miamba ya soka Tanzania, Simba na Yanga mechi itakayopigwa kesho saa 2:15 usiku.
Post a Comment