Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kikosi chake kiko safi na wanaendelea na mazoezi kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara Jumapili ijayo dhidi ya Mwadui FC.
Mwambusi anaeleza kuwa wachezaji waliokuwa majeruhi wote wamerejea kikosini isipokuwa Donald Ngoma ambaye bado hajarejea nchini kutoka Zimbabwe alipokwenda baada ya kupata msiba wa kaka yake.
"Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwani mahudhurio yamekuwa mazuri wachezaji waliokuwa majeruhi wamerejea na tayari wameanza kufanya mazoezi pamoja na kikosi kuelekea mchezo wa Jumapili kasoro Ngoma tu ambaye yeye bado hajarejea nchini baada ya kupata matatizo ya msiba wa kaka yake." Alisema Mwambusi
Post a Comment