0





Staa wa Liverpool, Philippe Coutinho amevunja rekodi kwa kusaini mkataba mpya wa kuitumika klabu hiyo utakaomwezesha kulipwa pauni 200,000 kwa wiki (zaidi ya shilingi milioni 560) ambazo hajawahi kulipwa mchezeaji yoyote katika timu hiyo.

Mkataba huo aliousaini Coutinho utamfanya abaki klabuni hapo hadi mwaka 2022.

Staa huyo aliyetua Anfield miaka minne iliyopita akitokea Inter Milan ameonyesha kiwango cha hali ya juu huku baadhi ya vilabu vya Ulaya wakiwemo Barcelona vikimmezea mate.

Baada ya kusaini kandarasi hiyo mpya, Coutinho amesema: 'Nina furaha kubwa kusaini mkataba mpya hapa. Ni klabu ambayo naikubali sana na hii inaonyehsa furaha yangu mahali hapa. Nitapambana kwa nguvu zangu zote ili kulipa fadhira nilizoonyesshwa.'

Post a Comment

 
Top