0


KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho amewapiga biti mashabiki wake kwamba mechi ya Jumapili dhidi ya Liverpool siyo 'matembezi ya kwenda kwenye ukumbi wa filamu' bali wajitokeze na kucheza pamoja na timu yao.

United wanaelekea katika mechi hiyo baada ya ushindi wao wa bao 2-0 jana usiku dhidi ya Hull City katika mchezo wa awamu ya kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Ligi (EFL).

Mourinho ameongeza kuwa kila mchezaji anatakiwa kufanya kazi ya ziada wakati wa mchezo huo dhidi ya Liverpool.


"Ni mechi muhimu sana kwetu, alisema kocha huyo. Tunapocheza vyema mashabiki pia hushirikiana nasi

"Tunaposhindwa kucheza vizuri ni vyema kwamba mashabiki hawapaswi kulalamika sana.

"Kila mtu anapenda mechi kubwa, wachezaji, makocha na mashabiki. Kila mmoja anapenda mechi kubwa, hivyo tuelekee katika mechi hiyo siku ya Jumapili kwa pamoja".

Post a Comment

 
Top